Jumapili, 26 Julai 2015

LESONI LEO:-“UHAMISHO" -Jumapili, Julai 26, 2015


Soma Isaya 39:5-7 na Danieli 1:1,2. Je, aya hizi zinahusianaje?
Danieli, ambaye jina lake humaanisha “Mungu ni hakimu wangu” alilazimishwa kutembea toka Yerusalemu, mji uliokuwa umeshindwa, hadi katika mji mkuu wa Babeli. Kitabu cha Danieli hutoa picha kidogo ya maisha yake katika ikulu za Babeli na Uajemi. Baada ya miaka mitatu ya “elimu” huko Babeli, Danieli aliajiriwa kama mtumishi wa serikali na mshauri wa mfalme. Kupitia uweza wa Mungu, alipanda juu kuliko hadhi ya kawaida ya mateka na kuwa mmisionari mstahiki katika yale mataifa makubwa mawili.

USOMAJI WA BIBLIA LEO:- MWANZO 15- Jumapili, Julai 26, 2015

Mwanzo 15

1 Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.

2 Abramu akasema, Ee Bwana MUNGU, utanipa nini, nami naenda zangu hali sina mtoto, na atakayeimiliki nyumba yangu ni huyu Eliezeri, Mdameski?

Jumamosi, 25 Julai 2015

IBADA YA SABATO YA LEO, Julai 25, 2015: - "MUNGU AMETUCHAGUA TUFANYWE WATOTO WAKE" - hubiri kutoka kwa Mchungaji Amos Lutebekela

WIMBO: Namba  142- NASIKIA MWITO

FUNGU KUU:,"kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. 5Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake." ( Waefeso 1:4 - 5)
UFAFANUZI:
Ni Mungu anayetuchagua na kutupatia uwezo wa kufanya kila jambo, hata tendo hili la kuingia kanisani katika sabato ya leo ni Mungu ndiyo amechagua, na hili hutokea mara tu pale tunapokubali uchaguzi huu uliotoka kwa Mungu yaani kuchaguliwa kuwa watoto wa Mungu.

LESONI 5:- WAMISIONARI UHAMISHONI - Julai 25 - 31, 2015

Sabato Mchana

Somo la Juma Hili: Danieli 1-12; Isaya 39:5-7; Danieli 2:44; Mathayo 24:14,15; Mwanzo 41.
Fungu la Kukariri: “‘Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa. ’” (Danieli 7:14).

Kama watu wa unabii, Waadventista wa Sabato huamini katika kurudi upesi kwa Yesu Kristo. Kuja kwake kutaifikisha dunia hii katika mwisho wake, na kuanzisha zama mpya ya ufalme wa milele wa Mungu, kama ilivyoelezwa ifuatavyo katika kitabu cha Danieli: “Na ufalme, na mamlaka, na ukuu wa ufalme, chini ya mbingu zote, watapewa watu wa watakatifu wake Aliye juu; ufalme wake ni ufalme wa milele, na wote wenye mamlaka watamtumikia na kumtii” (Dan. 7:27). Ufalme huu ndivyo utimilifu wa imani yetu; ni kile ambacho kitabu cha Waebrania (Ebr. 11:16) inakiita “nchi iliyo bora”, ambayo watu wote wa Mungu wa vizazi vyote waliisubiria kwa hamu, ambayo “mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu” (Waebrania 11:10).

Lakini kitabu cha Danieli pia ni kama mwongozo wa shughuli za umisionari. Katika kitabu hicho tunaweza kupata masomo kuhusu namna Mungu alivyoweza kuwatumia baadhi ya watu kushuhudia kwa wale waliokuwa katika ujinga wa kiroho na kiteolojia. Kupitia uaminifu wao na bidii yao, na imani thabiti, waumini hawa waliudhihirisha ukweli wa Mungu aliye hai kwa wale waliojua tu miungu ya uongo, na hivyo wakawapatia wale wapangani nao fursa ya kuwa na nafasi katika ufalme wa milele.

USOMAJI WA BIBLIA LEO- MWANZO 14 - Jumamosi , Julai 25, 2015


Mwanzo 14

1 Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu,

2 walifanya vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari.

3 Hawa wote wakakutana panapo bonde la Sidimu, kwenye Bahari ya Chumvi.

4 Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi.

5 Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,

Ijumaa, 24 Julai 2015

USOMAJI BIBLIA LEO:- MWANZO 13 - Ijumaa, Julai 24, 2015

Mwanzo 13

Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini.

2 Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu.

Alhamisi, 23 Julai 2015

USOMAJI WA BIBLIA LEO: - MWANZO 12 - Alhamisi, Julai 23, 2015

Mwanzo 12

Bwana akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha;

2 nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka;

LESONI YA ALHAMISI:- KILIO CHA NINAWI - Julai 23, 2015


Yona 4:1-11 huthibitisha kuwa kikwazo kikubwa kwa Mungu kumfanya nabii wake ahusike katika utume kwa ulimwengu hakikuwa umbali, upepo, mabaharia, samaki, au watu wa Ninawi.

KESHA LA ASUBUHI:- UKUTA WA MOTO DHIDI YA MAJARIBU - Alhamisi, Julai 23, 2015

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11.
Shetani anatafuta daima kuishawishi mioyo ya wanadamu kwa hila zake.
Yeye ndiye mwanzilishi mwamba; alipewa uwezo huo na Mungu, lakini akauharibu uwezo wake wote mtukufu kwa kuyapinga na kuyafanya mashauri yake yule Aliye juu sana yasiwe na maana yo yote....

Jumatano, 22 Julai 2015

LESONI JUMATANO, Julai 22, 2015- KIZAZI CHA NINAWI


Somo Yona 3. Ni ujumbe gani muhimu unapatikana hapa katika muktadha wa kushuhudia na uinjilisti?

"Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili,kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru." (Yona 3:1,2).

USOMAJI WA BIBLIA LEO Jumatano, Julai 22, 2015


Mwanzo 11

1 Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.

2 Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.

3 Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.

KESHA LA ASUBUHI: MKATE UNAOSHIBISHA - Jumatano, Julai 22, 2015

Mimi ndimi chakula [mkate] chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. 
Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.... 

Jumanne, 21 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI: Jumanne, Julai 21, 2015-MAJANI YA MTI ULE WA UZIMA

Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; 
yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
" Yohana 6:35. Ulimwengu unaangamia kwa kuikosa kweli, kweli ile safi, isiyoghoshiwa. Kristo ndiye ile kweli. Maneno yake ndiyo kweli. ----- MS 130, 1897.

USOMAJI WA BIBLIA LEO Jumanne, Julai 21, 2026

Mwanzo 9

1 Mungu akambariki Nuhu na wanawe, akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi.

2 Kila mnyama wa katika nchi atawaogopa ninyi na kuwahofu, na kila ndege wa angani: pamoja na vitu vyote vilivyojaa katika ardhi, na samaki wote wa baharini; vimetiwa mikononi mwenu.

Jumatatu, 20 Julai 2015

LESONI YA LEO JUMATATU Julai 20, 2015: Mmisionari wa Awali


"Ondoka, uende Ninawi!" lilikuwa ndilo agizo la Mungu kwa Yona. Katika Agano la Kale wito jwa kawaida ulikuwa "Njoni Sayuni." Mpango wa Mungu wa awali ulikuwa kwamba Isaeli wapate kuishi kivitendo kulingana na dini yao, kiasi cha kuwafanya Mataifa mengine wavutwe kuja kwao kutafuta ushauri (Isaya 56:70).

USOMAJI WA BIBLIA LEO Jumatatu, Julai 20, 2015.


Mwanzo 8

1 Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;

Jumapili, 19 Julai 2015

USOMAJI WA BIBLIA LEO Jumapili, Julai 19, 2015

Mwanzo 7
1 Bwana akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.

LESONI 4 : KISA CHA YOHANA, Julai 18-24, 2015

SABATO MCHANA
Sabato Mchana
Somo la Juma Hili: Yona 1-4; 2 Wafalme 14:25; Isaya 56:7; Isaya 44:8; Mathayo 12:40; Ufunuo 14:6-12.

Fungu la Kukariri: “‘Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yete’” (Matendo 10:34, 35).

Kisa cha Yona ni maelezo kuhusu nabii Mwebrania aliyekuwa akihudumu nje ya eneo alilokuwa analipenda.

Jumamosi, 18 Julai 2015

USOMAJI WA BIBLIA LEO Jumamosi, Julai 18, 2015

Mwanzo 6
1 Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao,

2 wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri; wakajitwalia wake wo wote waliowachagua.

HABARI PICHA KATIKA IBADA YA LEO SINZA SDA CHURCH

Mtumishi wa Mungu Ashery Anthony  akinena na waumini waliohudhuria ibada ya Sinza leo

Kwaya ya kanisa la Sinza Sauti Ya Nyikani ikimtukuza Mungu katika ibada ya leo 


WATATU WAMEJITOA KIKAMILIFU KWA AJILI YA UBATIZO KATIKA IBADA YA LEO ILIYOENDESHWA NA MZEE WA KANISA Mr. Ashery Anthony

Wa kwanza kutoka kulia ni Karani wa kanisa Mr. Joseph Kengera akiandikisha majina ya makamanda hao wa Yesu walijitoa kwa ubatizo katika ibada ya leo.
Ikiwa ni katika kutokuionea aya imani juu ya Yesu Kristo, vijana watatu leo wamemkataa shetani mbele ya washiriki wa kanisa la Sinza kwa kuamua kujitoa kikamilifu kwa ajili ya ubatizo wa maji mengi kupitia kanisa la waadventista wa Sabato Sinza.

SABATO YA LEO Julai 18, 2015: "TABIBU WA KWELI WA DHAMBI" hubiri kutoka kwa Mzee Ashery Anthony


WIMBO: Namba  111- TABIBU MKUU

FUNGU KUU:,"Na  kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi , atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye  haki kwafaa sana akiomba kwa bidii." ( Yakobo 5:15 -16)
Mzee wa Kanisa Ashery Anthony akihubiri katika ibada ya leo

Jumanne, 14 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI: HIVI NI KWELI TUNAJITOLEA MHANGA? Jumanne, Julai 14, 2015

Washangilie,wakufurahie, Wote wakutafutao.

Waupendao wokovu wako waseme daima, Atukuzwe BWANA. Zaburi 40:16. Wengi wanasema juu ya maisha ya Mkristo kuwa yanatuondolea anasa na raha za dunia.

Mimi nasema hayaondoi kitu chochote kinachofaa kukitunza. Je, kuna mashaka, umaskini, na dhiki anayopata Mkristo? Ndiyo, jambo hilo linatazamiwa katika maisha haya.

Jumatatu, 13 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI: KIPIMO CHA TABIA - Jumatatu, Julai 13, 2015

Lakini  hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana  na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 1 Timotheo 6:9,10.

Jumamosi, 11 Julai 2015

"USHINDI WA KURA YA HAPANA DHIDI YA KUWEKEWA MIKONO YA WAKFU WANAWAKE HAIBADILI SERA YA SASA YA KANISA" alisema Rais Ted Wilson

Divisheni ya Amerika ya kaskazini inasema itaendelea kuhamasisha wanawake kutumika katika huduma ya injili.

Rais wa Baraza kuu Ted N.C. Wilson alisema hapo jana kwamba kura iliyopigwa wiki hii kuhusu suala la kuwawekea mikono ya wakfu wanawake ilimaanisha “tumedumisha sera ya sasa.”

Alhamisi, 9 Julai 2015

MAREKEBISHO YA KIHISTORIA YA IMANI 28 ZA MSINGI ILI KUENDANA NA WAKATI WA SASA YAPITISHWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU 2015

Wajumbe wapitisha mabadiliko ya kihistoria ya Imani za Msingi za Kanisa la Waadventista wa Sabato
Ezekiel Adeleye, kutoka Divisheni ya Africa Magharibi ya kati , akipiga kura kupitisha Imani ya Msingi namba 1 kuhusu Maandiko matakatifu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kuendana na wakati wa sasa pamoja na kuimarisha uandishi wa imani hizo ili kueleweka kwa urahisi pasipo kubadili dhana kuu ya kila imani ya msingi.
Tangun ilipopitishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1980, Imani za Msingi zilikuwa hazijawahi kupitiwa upya tena ukiacha ile imani moja ya ziada iliyopitishwa mwaka 2005.

Hivyo idhini ya wajumbe wa Mkutano Mkuu siku ya jumanne, julai 7, 2015 kupitia upya tena Imani hizo ilikuwa ni hitimisho la mchakato wa miaka mitano ya upitiaji na uboreshaji upya wa Imani za Msingi za Kanisa la Waadventista wa Sabato.

HOJA YA KUWEKEWA MIKONO YA WAKFU WANAWAKE HAIJAPITISHWA

"Hakuna ushindi juu ya jambo hili," alisema MICHAEL L. RYAN. "Hakuna washindi wala walioshindwa."

Roho Mtakatifu ameongoza wajumbe wa kikao cha General Conference 2015 kupiga kura ya HAPANA, kuhusu suala la kuwawekea mikono ya wakfu kwa kazi takatifu wanawake.

Kwa kiasi cha kura 1381 za ndiyo, 977 za hapana, na 5 ambazo hazikupigwa, wajumbe kwa kura ya siri walimaliza mchakato wa miaka mitano kuhusu kwawekea mikono wanawake uliotawaliwa kwa majadiliano mazito na wakati mwingine kutumika hata kwa lugha kali za kuudhi.

Jumatano, 8 Julai 2015

TAARIFA YA MHAZINI MKUU KATIKA KIKAO CHA GC 2015, July 05, 2015 | San Antonio, Texas, United States of America | Robert Lemon

ROBERT LEMON
MHAZINI WA GENERAL CONFERENCE
Robert Lemon, Mhazini anayemaliza muda wake, aliwasilisha Taarifa ya Mhazini kwa mwaka 2015 mnamo siku ya Ijumaa, Julai 3.

ZAKA NA SADAKA


Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, zaka ya kila mwaka duniani kote imeongezeka kwa 31% kutoka dola za kimarekani bilioni 1.85 mwaka 2009 hadi dola za kimarekani bilioni 2.43 mwaka 2014.

USOMAJI WA BIBLIA LEO Alhamisi, Julai 8, 2015

Ufunuo 17

Kahaba Mkuu na Mnyama

1 Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye vile vitasa saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;2ambaye wafalme wa nchi wamezini naye, nao wakaao katika nchi wamelevywa kwa mvinyo ya uasherati wake.

MCHUNGAJI GEOFREY MBWANA ACHAGULIWA TENA KUWA MAKAMU WA RAISI WA GENERAL CONFERENCE

Pr. Geoffrey Mbwana
Makamu wa Raisi wa General Conference 2015-2020







Jumanne, 7 Julai 2015

MSHIRIKI WA KANISA LA USHINDI SDA ACHAGULIWA KUWA MJUMBE WA BODI YA UKAGUZI YA GENERAL CONFERENCE 2015 - 2020

 
ESTHER ABAYO
MSHIRIKI WA KANISA LA USHINDI SDA, DAR ES SALAAM , TANZANIA
Esther Abayo ambaye ni mshirirki wa kanisa la Waadventista wa Sabato Ushindi Dar-es-Salaam, Tanzania amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ukaguzi ya General Conference (GCAS) 2015-2020, katika kikao cha Baraza Kuu la Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni (General Conference Session ) 2015.

USOMAJI WA BIBLIA LEO

JUMANNE, JULAI 7 , 2015

Ufunuo 15

Malaika Saba wenye Mapigo Saba ya Mwisho

1 Kisha nikaona ishara nyingine katika mbingu, iliyo kubwa, na ya ajabu; malaika saba wenye mapigo saba ya mwisho; maana katika hayo ghadhabu ya Mungu imetimia.

KESHA LA ASUBUHI

NI LAANA AU MBARAKA?

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba.
Mathayo 6:19. 
Hazina ni vitu vile vinavyoujaza sana moyo, na kuchota mawazo yote, na kumwacha nje Mungu na ile kweli.

Jumatatu, 6 Julai 2015

Mchungaji Bina Afungua Rasmi Mkutano wa TAiN-Tanzania Adventist Internet Network, 2015

Monday, June 22, 2015


MOTTO: TAIN 2015, UBUNIFU ZAIDI.

Mafundi mitambo wakiweka mambo sawa tayari kwa kuanza Mkutano.
Mchungaji HARUNI KIKIWA akiwa anaongoza Uimbaji katika Mkutano.
Somo la Ufunguzi wa mkutano wa TAIN 2015, limetolewa na Mch. Bina kutoka ECD likijengwa kutoka katika kitabu cha Mathayo 24. Aidha amesisitiza viongozi wa Tehama kuwa makini kwani hizi ni siku za mwisho.
"Bwana atakomesha maisha yetu siku moja na hivyo tunapaswa kutengeneza maisha yetu na sio kujiinua kwa mafanikio yetu" Amesema Mch. Bina

MBARAKA WA MASTER GUIDE 2 WAPYA NDANI YA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO SINZA


Master Guide Rebecca
Master Guide Malekela
Miongoni mwa makanisa yaliyofanikiwa kuhitimisha Master Guide mafunzoni katika kambi la mafunzo kwa vijana huko Chimala, Mbeya ni Kanisa la Sinza SDA kutoka Dar es Salaam.

MATUKIO KATIKA PICHA YA KAMBI LA CHIMALA, MBEYA JUNI 21 - 28, 2015

Master Guide Kelvin Peter(Aliyevaa Uniform) akipata chai na Vijana wa kambi
Balozi Neria, Neema, na Suzy kutoka kanisa la Sinza pamoja na AY Mariamu wakifuatilia mafunzo kwa makini

Jumamosi, 4 Julai 2015

ALICHOSEMA TED N.C. WILSON MUDA MFUPI MARA BAADA YA KUCHAGULIWA KUWA RAISI TENA

“Hakuna anayeweza kushughulikia nafasi hii isipokuwa kwa kuongozwa moja kwa moja  na Uongozi wa Mungu.Hivyo ni uzoefu wa kujishusha sana."

WAJUMBE WA KIKAO CHA GC, 2015 WATUMIA MFUMO MPYA WA KIELECTRONIC KUPIGA KURA

BOFYA HAPA KUONA VIDEO
Mchungaji Dr. Blasiusc Luguri akisifia mfumo mpya wa kielectronic uliotumika katika kuchagua viongozi wa GC mwaka huu 2015.

YALIYOJILI SIKU YA PILI KATIKA KIKAO CHA GENERAL CONFERENCE

UNION CONFERENCE MPYA 35 ZAPITISHWA KATIKA KIKAO CHA GC 2015

Ted N.C. Wilson akihutubia wajumbe wa kikao cha Mkutano Mkuu siku ya kwanza ya kikao.

TED N.C. WILSON ACHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA WAADVENTISTA WASABATO ULIMWENGUNI

Ted N.C. Wilson speaks to delegates shortly after his reelection as General Conference president. [Photo ©2015 Adventist Review / ANN. Photos by Josef Kissinger]

WILSON ACCEPTS THE NEW FIVE-YEAR TERM WITH “QUIET RESPECT AND HUMILITY.”

Delegates overwhelming elected incumbent General Conference president Ted N.C. Wilson to another five years in office on Friday.
An estimated 90 percent of some 1,900 registered delegates voted in favor of continuing Wilson in his position as leader of the Seventh-day Adventist world church after a 37-minute discussion at the General Conference session in San Antonio, Texas.

SIKU YA UFUNGUZI, GC SESSION 2015

USOMAJI WA BIBLIA LEO

Ufunuo 9

1Kisha, malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. 2Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la kuzimu, kukatoka moshi wa tanuri kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa kuzimu. 3Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani, wakapewa nguvu kama ya nge.

KESHA LA ASUBUI: HAKUNA CHA THAMANI MNO USICHOWEZA KUMPA MUNGU, Julai 4, 2025.

Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee. Waebrania 11:17.

Jaribio la Ibrahimu lilikuwa kali mno ambalo lilipata kumjia mwanadamu. Angeshindwa chini ya jaribio hilo, asingeweza kuandikwa kamwe kama babawa wenye imani....

TAARIFA YA KATIBU MTENDAJI KATIKA KIKAO CHA GC 2015

FULL TEXT: 2015 GC SESSION SECRETARY'S REPORT


FULL TEXT: 2015 GC Session Secretary's Report
G. T. Ng is the executive secretary of the Seventh-day Adventist world church. In this file photo, he is addressing Spring Meeting delegates at the denomination's world headquarters in Silver Spring, Maryland, United States, on Wednesday, April 9, 2014. [photo: Ansel Oliver]

WAJUMBE WALIOCHAGULIWA KUINGIA KATIKA KAMATI YA UTEUZI KATIKA KIKAO CHA GC 2015

General Conference Session delegates select 2015 nominating committee members
July 03, 2015 | San Antonio, Texas | ANN/Adventist Review Staff
Ifuatayo chini ni orodha ya walioteuliwa kuingia katika kamati ya uteuzi ya kikao cha GC 2015. Ni wajumbe 252 wa kamati watawajibika kuchagua majina yatakayochaguliwa kwa ajili ya Viongozi wa juu wa Kanisa.

KANISA LIMEKUBALI KUREJEA KWA KUNDI LILILOJITENGA NA KANISA NCHINI HUNGARY TANGU MWAKA 1975

World Church welcomes back Hungarian splinter group

Baada ya miaka 40 ya utengano, sasa yametimia katika kikao cha Mkutano Mkuu wa kanisa mwaka 2015, baada ya Kanisa ya ulimwenguni kukubali na kupokea maridhiano ya kihistoria kati ya kanisa la Waadventista Hungary na Kundi la Breakaway linalojulikana kama KERAK.

Kanisa la Waadventista wa Sabato katika nchi ya Hungary lilipata mpasuko mnamo mwaka 1975, takribani miaka 40 sasa iliyopita,
Kanisa nchini Hungary lina jumla ya washiriki 4,629 wanaoabudu katika makanisa 104 wakati kundi la KERAK lina jumla ya washiriki 1,500 hadi 1,800.

Ijumaa, 3 Julai 2015

LESONI: TABIA YA MUNGU YA UMISIONARI

Ijumaa: Julai 3, 2015


Jifunze Zaidi: “Tume gusia vipengele kadhaa vya tabia ya Mungu ya umisionari. Utume ni shughuli muhimu ya Utatu Mtakatifu. Kimsingi, utume unahusianishwa hasa na Yesu Kristo, ambaye kufanyika kwake mwili ni kitovu cha imani na utume wa Kikristo. Kwa njia ya maisha na kifo chake, Yesu amefungua njia kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote . Sisi kama wafuasi wake , wamisionari wake , tunapaswa kuwajulisha watu habari njema kuhusu kile amabacho Yesu amefanya kwa ajili yao.

Neno la leo 

Ijumaa, Julai 3, 2015

Ufunuo 7
Kupigwa mhuri kwa watu 144,000 wa Israeli
1Baada ya hayo nikawaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za dunia, wakishika pepo nne za dunia ili upepo usivume hata kidogo: Wala katika nchi, wala baharini, wala kwenye miti. 2Kisha, nikamwona malaika mwingine akipanda juu kutoka mashariki, akiwa na mhuri wa Mungu aliye hai. Akapaza sauti na kuwaambia hao malaika wanne waliokabidhiwa jukumu la kuiharibu nchi na bahari, 3“Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.” 4Kisha, nikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu 144,000 wa makabila yote ya watu wa Israeli. 5Kabila la Yuda, watu 12,000; kabila la Reubeni, 12,000; kabila la Gadi, 12,000; 6kabila la Asheri, 12,000; kabila la Naftali, 12,000; kabila la Manase, 12,000; 7kabila la Simeoni, 12,000; kabila la Lawi, 12,000; kabila la Isakari, 12,000; 8kabila la Zebuluni, 12,000; kabila la Yosefu, 12,000; na kabila la Benyamini, 12,000.
Umati wa watu wa kila taifa
9Kisha, nikatazama, nikaona umati mkubwa wa watu wasiohesabika: Watu wa kila taifa, ukoo, jamaa na lugha. Nao walikuwa wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo, wamevaa mavazi meupe na kushika matawi ya mitende mikononi mwao. 10Wakapaza sauti: “Ukombozi wetu watoka kwa Mungu wetu aketiye juu ya kiti cha enzi, na kutoka kwa Mwanakondoo!” 11Malaika wote wakasimama kukizunguka kiti cha enzi, wazee na wale viumbe hai wanne. Wakaanguka kifudifudi mbele ya kiti cha enzi, wakamwabudu Mungu, 12wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukrani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu, milele na milele! Amina!”
13Mmoja wa hao wazee akaniuliza, “Hawa waliovaa mavazi meupe ni watu gani? Na wametoka wapi?” 14Nami nikamjibu, “Mheshimiwa, wewe wajua!” Naye akaniambia, “Hawa ni wale waliopita salama katika ule udhalimu mkuu. Waliyaosha mavazi yao katika damu ya Mwanakondoo, yakawa meupe kabisa. 15Ndiyo maana wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Humtumikia Mungu mchana na usiku katika hekalu lake; naye aketiye juu ya kiti cha enzi atatandaza hema lake juu yao kuwalinda. 16Hawataona tena njaa wala kiu; jua wala joto kali halitawachoma tena,17kwa sababu Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji ya uhai. Naye Mungu atayafuta machozi yote machoni mwao.”
Ufunuo 8
Mhuri wa saba
1Na Mwanakondoo alipouvunja mhuri wa saba, kukawa kimya mbinguni kwa muda wa nusu saa. 2Kisha, nikawaona wale malaika saba wanaosimama mbele ya Mungu wamepewa tarumbeta saba.
3Malaika mwingine akafika, anachukua chetezo cha dhahabu, akasimama mbele ya madhabahu ya kufukizia ubani. Naye akapewa ubani mwingi autoe sadaka pamoja na sala za watu wote wa Mungu juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi. 4Moshi wa ubani ukapanda juu, pamoja na sala za watu wa Mungu kutoka mikononi mwake huyo malaika aliyekuwa mbele ya Mungu.5Kisha, malaika akakichukua hicho chetezo, akakijaza moto wa madhabahuni, akakitupa duniani. Kukawa na ngurumo, sauti, umeme na tetemeko la ardhi.
Tarumbeta
6Kisha, wale malaika saba wenye tarumbeta saba wakajiweka tayari kupiga mbiu ya mgambo.
7Malaika wa kwanza akapiga tarumbeta yake. Mchanganyiko wa mvua ya mawe na moto pamoja na damu ukamwagwa juu ya nchi. Theluthi moja ya nchi ikaungua, theluthi moja ya miti ikaungua na majani yote mabichi yakaungua.
8Kisha malaika wa pili akapiga tarumbeta yake. Na kitu kama mlima mkubwa unaowaka moto kikatupwa baharini. Theluthi moja ya bahari ikawa damu, 9theluthi moja ya viumbe vya baharini vikafa, na theluthi moja ya meli zikaharibiwa.
10Kisha, malaika wa tatu akapiga tarumbeta yake. Na nyota kubwa ikiwaka kama bonge la moto ikaanguka kutoka mbinguni na kutua juu ya theluthi moja ya mito na chemchemi za maji. 11(Nyota hiyo inaitwa “Uchungu.”) Basi, theluthi moja ya maji yakawa machungu; watu wengi wakafa kutokana na maji hayo, kwa sababu yaligeuka kuwa machungu.
12Kisha, malaika wa nne akapiga tarumbeta yake. Ndipo theluthi moja ya jua, ya mwezi na ya nyota ikapata pigo; hata mwangaza ukapoteza theluthi moja ya mng'ao wake. Theluthi moja ya mchana ikakosa mwanga, hali kadhalika na theluthi moja ya usiku.
13Kisha, nikatazama, nikasikia tai akiruka juu kabisa angani, anasema kwa sauti kubwa, “Ole, ole, ole kwa wanaoishi duniani wakati malaika watatu waliobaki watakapopiga tarumbeta zao!”