Jumapili, 30 Agosti 2015

SOMO LA ASUBUHI LEO Jumapili, Agosti 30, 2015

VIJANA WANAPASWA KUMTETEA KRISTO

Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu
atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika
watakatifu. Luka 9:26.

Sikuzote umtetee Kristo. Kwa maneno, kwa roho, na kwa matendo yako, uwe shahidi
wake. Anakupenda, naye anataka kukupa wewe neema yake nyingi, ili nawe upate
kuwapa wengine.... Kristo amekununua kwa damu yake mwenyewe. Basi kila mahali,
nyakati zote na chini ya hali zote, umtetee Yesu. Kumbuka kwamba kwa njia hiyo
utakuwa na mvuto wenye nguvu nyingi sana juu ya wote unaoshirikiana nao....

Jumanne, 25 Agosti 2015

SOMO LA ASUBUHI LEO Jumanne, Agosti 25, 2015

CHUNGA HATUA YAKO! 

  
 Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike. Mithali 4:26.

"Mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka," asema mtume, "ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe." Waebrania 12:13. Njia ile inayokwenda mbali na Mungu, yaani, mbali na kanuni yake ya haki, takatifu, na kamilifu [Amri Kumi], sikuzote imepotoka na ni ya hatari. Hata hivyo... wengi wamekuwa wakienda katika njia hiyo ya uasi. Katika mifano mingi [inayofahamika], hawakuanza vizuri katika utoto na ujana wao, nao wamezifuata njia hizo potofu katika safari yao yote. Sio tu kwamba wao wenyewe wamekosa kwa kuiacha njia ile ya kweli, bali kwa mvuto wa mfano wao wengine vile vile wamepotoshwa kutoka katika njia ile dhahiri iliyonyoka, nao wamefanya makosa ya kufisha....