Jumapili, 30 Agosti 2015

SOMO LA ASUBUHI LEO Jumapili, Agosti 30, 2015

VIJANA WANAPASWA KUMTETEA KRISTO

Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu
atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika
watakatifu. Luka 9:26.

Sikuzote umtetee Kristo. Kwa maneno, kwa roho, na kwa matendo yako, uwe shahidi
wake. Anakupenda, naye anataka kukupa wewe neema yake nyingi, ili nawe upate
kuwapa wengine.... Kristo amekununua kwa damu yake mwenyewe. Basi kila mahali,
nyakati zote na chini ya hali zote, umtetee Yesu. Kumbuka kwamba kwa njia hiyo
utakuwa na mvuto wenye nguvu nyingi sana juu ya wote unaoshirikiana nao....


Ni haki yako kukua katika neema daima, ukizidi sana katika kumjua na kumpenda
Mungu, endapo wewe utahifadhi umoja wako na Kristo, basi, hapo itakuwa ni haki yako
kuifurahia. Kwa imani ya kawaida inayonyenyekea mwombe Bwana aufungue ufahamu
wako, ili upate kutambua na kuyathamini mambo yale ya thamani yaliyo katika Neno lake. 
Hivyo unaweza kukua katika neema, kukua ukiwa na imani ya kawaida, inayomtumainia yeye. 
Ndipo nuru yako itakapoangaza kwa wote unaoshirikiana nao. Moyo wako uukaze umwelekee Mwokozi....

Uwe na hakika kwamba maisha yako ya kiroho hayawi duni, dhaifu, yasiyo na ufanisi
wo wote. Wako wengi wanaohitaji maneno na kielelezo cha Mkristo. Udhaifu na
kusitasita huchokoza mashambulio ya yule adui, na ye yote yule anayeshindwa kukua
kiroho, katika ujuzi wa ile kweli na haki, mara kwa mara atashindwa na yule adui. -----
Letter 36, 190l.

Uso wako na uakisi tabia ya Bwana. Zungumza juu ya fadhili zake na simulia juu ya
uweza wake. Hapo ndipo nuru yako itakapozidi kuangaza kwa wazi zaidi na zaidi. Juu ya
maonjo yako na kukata tamaa kwako yataonekana maisha yako ya kidini yaliyo safi na
yenye afya. ----- Letter 121, 1904.

Hakuna kikomo cha mvuto wa mjumbe yule wa kibinadamu anayeivaa nira ile pamoja
na Kristo. Kila siku anajifunza maisha ya Kristo na kuyafananisha maisha yake kulingana
na kielelezo hicho cha mbinguni.... Ni kwa kuonekana roho ile ya Kristo katika maneno
na matendo yetu ulimwengu unajua ya kuwa sisi tumekuwa pamoja na Yesu, ya kuwa
sisi tu watoto wa Mungu. Tabia halisi ya dini yetu inapatikana... katika roho ya tulivu, ya
upole, na amani tunayoionyesha. ----- Letter 34, 1894.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...