Alhamisi, 9 Julai 2015

MAREKEBISHO YA KIHISTORIA YA IMANI 28 ZA MSINGI ILI KUENDANA NA WAKATI WA SASA YAPITISHWA NA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU 2015

Wajumbe wapitisha mabadiliko ya kihistoria ya Imani za Msingi za Kanisa la Waadventista wa Sabato
Ezekiel Adeleye, kutoka Divisheni ya Africa Magharibi ya kati , akipiga kura kupitisha Imani ya Msingi namba 1 kuhusu Maandiko matakatifu.
Marekebisho hayo yamefanyika ili kuendana na wakati wa sasa pamoja na kuimarisha uandishi wa imani hizo ili kueleweka kwa urahisi pasipo kubadili dhana kuu ya kila imani ya msingi.
Tangun ilipopitishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1980, Imani za Msingi zilikuwa hazijawahi kupitiwa upya tena ukiacha ile imani moja ya ziada iliyopitishwa mwaka 2005.

Hivyo idhini ya wajumbe wa Mkutano Mkuu siku ya jumanne, julai 7, 2015 kupitia upya tena Imani hizo ilikuwa ni hitimisho la mchakato wa miaka mitano ya upitiaji na uboreshaji upya wa Imani za Msingi za Kanisa la Waadventista wa Sabato.

Hakuna marekebisho yoyote yatakayobadili Imani yoyote ile ya Msingi, bali ni kuiboresha na kuongeza mkazo wa kimaandishi, Rais Ted N.C Wilson aliwahakikishia wajumbe mwanzoni kabisa mwa majadiliano., "Hatubadili Imani zetu za Msingi," alisema Wilson. "Tunajaribu tu kuiboresha na kuifanya ieleweke vizuri na kwa urahisi zaidi."

Kamati ya mapitio ilifanyia marekebisho Imani 21 za Msingi kati ya imani 28, na Artur A. Stele makamu mwenyekiti na Mwenyekiti wa kamati hiyo aliwasilisha mabadiliko hayo kwa wajumbe.

Mengi ya mabadiliko hayo ni madogo madogo, kama vile kuondolewa kwa neno "ambayo"yaani ("which") na kuwekwa neno "kuwa"yaani ("that") kutafakari matumizi ya maneno kwa wakati wa sasa kwa mfano matumizi ya neno "mtu"(man) kuwa watu(people)  na neno "watu"(mankind) kuwa ubinadamu(humanity) kwa lengo la kuhusisha jinsia zote.

Wajumbe waliongeza ufafanuzi katika Imani ya 23 kwamba ndoa ni kati ya mwanamke na mwanaume.

Siku ya jumatatu wajumbe walijadili na kupitisha jumala ya Imani 24 mmoja baada ya mwingine kwa kuipigia kura , na kuhusu Imani 4 yaani Maandiko Matakatifu(Imani 1), Uumbaji(Imani 6), Vita kuu(Imani 8), na Huduma ya patakatifu pa patakatifu(Imani 24) zilirudishwa kwa kamati ya mapitio kwa kufanyiwa kazi zaidi.

Siku ya jumanne kamati ilirudi ikiwa imefanyia kazi maoni yaliyotolewa na wajumbe, kwa siku zote hizo mjadala mkubwa ulitawaliwa sana na hoja kuhusu Imani juu ya Uumbaji na Maandiko Matakatifu.

Kwenye uumbaji msuguano ulikuwa juu ya kuweka neno "hivi karibuni" ili kuonesha ni lini dunia iliumbwa na kuweka maneno "siku sita halisi" ili kuonesha urefu wa juma la uumbaji.ni juu ya Imani  ya Uumbaji na Maandiko Matakatifukuweka neno "hivi karibuni"

Kwenye Maandiko Matakatifu hoja ilikuwa kuweka maneno "waandishi walioongozwa" badala ya maneno "watu watakatifu wa Mungu"

Baadhi ya wajumbe walitofautisha pia kati ya neno "mtunzi" na "mwandishi", wakisema Mungu alikuwa mtunzi wa Biblia nzima na binadamu walikuwa waandishi wake. Wajumbe wengine walionyesha wasiwasi juu ya uwekaji wa neno "waandishi" badala ya neno "wanaume" wakisema ni wanaume tu waliandika biblia hivyo hakuna haja ya kuhusisha lugha ya ujumla kuonyesha jinsi zote zinahusika.

Kwa namna ya urahisi wajumbe walikubali mapendekezo ya marekebisho ya mwishoni, mjadala ukafungwa.

Stele, mwenyekiti wa kamati ya mapitio, pia alitangaza siku hiyo ya jumanne kwamba Baraza kuu limepanga kuchapisha kitabu rahisi kusomeka na kueleweka kitakachobeba Imani za Msingi 28. Aliongea hayo baada ya baadhi ya wajumbe kutoka divisheni ya ulaya kueleza kuwa wabatizwa wapya na vijana wa kiadventista wanapata ugumu kuelewa Imani hizo katika uandishi wake wa sasa. Stele alisisitiza Imani kuja kuandikwa katika lugha ya kisasa kwa lengo la kufikia kizazi kipya.

Stele alitambua kwamba maandiko ya sasa ya Imani za Msingi "yanaweza yasiwe chombo bora cha injili" lakini, aliongeza, "Tumedhamiria kufanya kazi juu ya kitabu ambacho kitatumia lugha ya kueleweka kwa kizazi cha vijana.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...