Jumanne, 7 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI

NI LAANA AU MBARAKA?

Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba.
Mathayo 6:19. 
Hazina ni vitu vile vinavyoujaza sana moyo, na kuchota mawazo yote, na kumwacha nje Mungu na ile kweli.
Mwokozi wetu alitoa onyo dhahiri dhidi ya kuhodhi [kujilimbikizia] hazina za ulimweingu huu.
Matawi yote ya biashara, kazi za aina zote, ziko chini ya uangalizi wa jicho la Mungu; na kila Mkristo amepewa uwezo wa kufanya kitu fulani katika kazi yake Bwana. 
Si kitu kama mtu anafanya shughuli zake za kazi shambani, katika bohari, au katika chumba cha mahesabu, watu watawajibika kwa Mungu kwa matumizi ya busara na uaminifu ya talanta zao. 
Wanawajibika sawasawa kwa kazi YAO, kama vile mchungaji anayehudumu kwa neno na mafundisho awajibikavyo kwa kazi yake.... 
Mali inayowekwa katika hazina hapa duniani itakuwa ni laana tupu, lakini kama ikitumika katika kuijenga kazi ya ile kweli, ili Mungu apate kuheshimiwa, na roho zipate kuokolewa, basi, hapo haitakuwa laana, bali mbaraka. 
Mali ni ya muhimu katika kuiendeleza kila kazi iliyo nzuri; na kama vile watu wengine walivyopewa uwezo zaidi wa kupata mali kuliko wengine, basi, wangezitoa talanta zao kwa hao watoao riba, ili Bwana apate iliyo yake, pamoja na faida, hapo atakapokuja.... 
Wale walio tayari na wanaotaka kuweka mali yao katika kazi ya Mungu, watabarikiwa katika juhudi zao za kupata fedha.
Mungu aliumba chimbuko hilo la utajiri. 
Alitupa mwanga wa jua, na umande, na mvua, na kuifanya mimea kusitawi.
Aliwabariki wanadamu kwa kuwapa nguvu za akili na mwili, na kuwawezesha kujipatia mali, ili kazi yake ipate kuendelezwa na wale wanaojiita kuwa ni watoto wake. 
Maskini wametuzunguka kila upande, na Mungu anatukuzwa, maskini na wanaoteseka wanaposaidiwa na kufarijiwa. Si dhambi kupata na kumiliki mali kama mawakili wake Mungu, tukiishikilia tu mpaka pale atakapoitaka kwa mahitaji ya kazi yake. ----- RH, Sept. 18, 1888. 
Yatupasa kukumbuka daima kwamba sisi tumeingia ubia pamoja na Mungu. Kazi yake na kusudi lake hudai kupewa kipaumbele katika fikira zetu. ----- MS 13, 1896.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...