Ijumaa, 3 Julai 2015

LESONI: TABIA YA MUNGU YA UMISIONARI

Ijumaa: Julai 3, 2015


Jifunze Zaidi: “Tume gusia vipengele kadhaa vya tabia ya Mungu ya umisionari. Utume ni shughuli muhimu ya Utatu Mtakatifu. Kimsingi, utume unahusianishwa hasa na Yesu Kristo, ambaye kufanyika kwake mwili ni kitovu cha imani na utume wa Kikristo. Kwa njia ya maisha na kifo chake, Yesu amefungua njia kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote . Sisi kama wafuasi wake , wamisionari wake , tunapaswa kuwajulisha watu habari njema kuhusu kile amabacho Yesu amefanya kwa ajili yao.
“Kanisa la Kristo duniani lilianzishwa kwa makusudi ya umisionari, na Bwana ana shauku ya kuliona kanisa zima likiwa linabuni njia na mbinu ambazo kupitia hizo wakubwa kwa wadogo, matajiri kwa maskini , wataweza kuusikia ujumbe wa kweli. Sivyo wote walioitwa kwa umisionari katika nchi za mbali, lakini wote wanaweza kufanya kitu Fulani kupitia maombi yao na karama zao ili kusaidia kazi ya umisionari.” Ellen G. White,Testimonies for the Church,vol.6,uk.29.

Maswali ya Kujadili:

1. Tafakari kuhusu chimbuko la viumbe. Kwa nini kujifunza chimbuko la viumbee ni muhimu? Je, kujua chimbuko letu kunatusaidiaje kujitambua sisi ni nani na kusudi letu la kuwapo ni lipi hasa?

2. Nukuu ifuatayo hutusaidiaje kuelewa kuwapo kwa uhuru wa uchaguzi, upendo , na uovu katika dunia yetu? “Hivyo, kama Mungu anataka kuumba viumbe wenye pendo (wenye kuakisi upendo wake), inamlazimu aumbe viumbe huru ambao wanaweza kusababisha maumivu na uovu ulimwenguni kutokana na chaguzi zao. Nguvu ya upendo na uhuru humtaka Mungu aruhusu fursa ya sisi kukua katika upendo kupitia uhuru wetu wa kibinadamu. Njia pekee ya Mungu kutoruhusu viumbe huru wachague matendo mabaya ni kujizuia kabisa asiumbe viumbe walio na upendo.” Robert J.Spitzer, New Proofs for the Existence of God: Contributions of Contemporary Physics and Philosophy, Kindle Edition (Eerdmans Pub. Co..,2010 ), uk.233.

3. Kifo cha Yesu kilikuwa nitendo la mara moja tu ambalo lilitokea katika taifa moja dogo ndani ya himaya kubwa sana ya Dola ya Kirumi yapata miaka elfu mbili iliyopita. Lakini tukio hili lina umuhimu wa milele kwa kila mwanadamu. Ni wajibu gani uko juu yetu, sisi ambao tunalijua tendo hilo na maana yake, kuwaelezea wale wasiojua habari hizo? Je,watajifunzaje endapo wale wanaojua hawawaambii?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...