MABWAWA MAKUBWA YA MUNGU
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba
dunia, Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu. (Zaburi 90:2).
Baba yetu wa Mbinguni ametupatia ishara
nyingi zinazoonyesha ukuu wake na utukufu wake. Jambo hilo ni hivyo hasa kwa
kiwango cha kustaajabisha katika sehemu hizi za milima....* Mandhari mbalimbali
katika milima hii mirefu sana na miinuko yake yenye miamba, makorongo ya milima
hii yenye kina kirefu pamoja na vijito vyake vya maji vinavyokwenda kasi na
kupiga kelele toka juu ya milima hii, ... maji yake yakipasuka yanapogonga
miamba, na kutawanyika katika rasharasha kama mtandio, huifanya mandhari hiyo
kuwa nzuri kupita kiasi na yenye utukufu ajabu....
Milima ina hazina zenye mibaraka ambayo
Muumbaji amewapa wakazi wa dunia hii. Ni tofauti inayoonekana juu ya uso wa
nchi, milimani, katika nyanda tambarare, na mabondeni, ambayo inafunua hekima
na uweza wa huyo Mtendakazi Bingwa Mkuu. Na wale ambao wangetaka kuiondolea
mbali kutoka katika dunia hii miamba hiyo na milima, makorongo yasiyokaliwa na
watu pamoja na vijito vinavyopiga kelele viendavyo kasi, na magenge marefu
----- hao akili zao ... ni finyu mno kuweza kufahamu utukufu wa Mungu ulivyo.
Mungu, Mjenzi Mkuu, ameijenga milima hii
mirefu sana, ambayo mvuto wake juu ya hali ya hewa ni mbaraka kwa ulimwengu
wetu. Inavuta kutoka mawinguni unyevu mwingi unaourutubisha udongo. Safu za
milima ni mabwawa makubwa ya Mungu, yanayoipatia bahari maji yake. Hizo ndizo
vyanzo vya chemchemi, vijito, na mito midogo ya maji baridi, pamoja na mito
mikubwa. Zinapokea, kwa njia ya mvua na theluji, mvuke uliojaa hewani, na
kuusafirisha kwenda chini kwenye nyanda kame, tambarare.
Tungeiangalia milima hiyo
isiyokuwa na umbo linganifu kama chemchemi za Mungu zenye mibaraka ambazo
kutoka kwazo hububujika maji ya kukidhi mahitaji ya viumbe vyote vilivyo hai.
Kila wakati ninapoitazama milima hiyo najisikia moyoni mwangu kujawa na
shukrani kwa Mungu....
Kila kitu kinachotuzunguka hutufundisha sisi siku kwa siku mafundisho ya
upendo wa Baba yetu na ya uweza wake, na ya Sheria zake zinazotawala viumbe
vyake vya asili, ambazo ndizo msingi wa serikali zote mbinguni na duniani.
----- MS 62, 1886.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...