Jumanne, 8 Septemba 2015

SOMO LA ASUBUHI LEO

CHUNGA MAPENZI YAKO.


Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 2 Wakorintho 6:14.

Ningependa kukuonya* ujilinde kuhusu ni wapi unayaweka mapenzi yako.... Kumbuka kwamba maisha yako ni mali yake Yesu, na ya kwamba haikupasi kuishi kwa ajili ya nafsi yako tu. Haikupasi kuingia katika uhusiano wa ndoa na mtu asiyekuwa muumini, maana kwa kufanya hivyo, unafanya kinyume kabisa na kile alichoagiza Yesu. Waepuke wale wasioyaheshimu mambo ya dini. Mwepuke yule apendaye kukaa kivivu; mwepuke yule anayeyadhihaki mambo matakatifu. Epuka kushirikiana na yule anayetumia lugha chafu, au mwenye mazoea ya kutumia hata gilasi moja tu ya kileo kikali. Usisikilize posa ya mtu ambaye hautambui wajibu wake kwa Mungu.

Kweli safi, inayoitakasa nafsi, itakupa ujasiri wa kuzikata kamba zinazokufunga kwa mwenzi wako anayekupendeza sana ambaye unamjua kuwa hampendi wala hamchi Mungu, wala hajui cho chote juu ya kanuni za haki ile ya kweli. Sikuzote tunaweza kuvumilia udhaifu wa rafiki yetu na ujinga wake, bali maovu yake kamwe. Usiolewe kamwe na mtu asiyeamini.

Mimi nanena kwako Neno la Mungu tu, maana yeye anasema kwa nguvu ya kwamba muungano kama huo utakuwa na matokeo ya kuuvuta moyo wako mbali hata usiweze kumpenda na kumtumikia [Mungu].... Wewe kama mtoto wa Mungu, unaruhusiwa kufanya mkataba wa ndoa katika Bwana tu.... Endapo utakubali kuunganisha maisha yako na ya yule asiyeamini, basi, utakuwa unalidharau neno la Mungu na kuihatarisha roho yako....

Maisha yako ni kitu cha thamani mno kuweza kuyafanya kana kwamba yana thamani kidogo sana. Kalvari inakushuhudia wewe juu ya thamani ya roho yako. ----- Letter 51, 1894.

Hebu kila hatua unayochukua kuelekea kwenye muungano wa ndoa yako iwe ya staha, isiwe ya anasa, isiwe ya kujipamba kwa nje, iwe nyofu, kisha iwe na kusudi la dhati ili kumpendeza na kumheshimu Mungu. Ndoa inaathiri maisha ya baadaye katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ule ujao. Mkristo mwaminifu hatafanya mipango yo yote ambayo Mungu hawezi kuikubali.... Mfanye Kristo kuwa mshauri wako. Jifunze neno lake kwa maombi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...