MATENDO MEMA HUONGEZEKA KWA KUYAFANYIA MAZOEZI
Katika mambo yote
ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika
mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, na maneno yenye uzima
yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa
hana neno baya la kunena juu yetu. Tito 2:7, 8.
Mkristo mwenye afya,
anayeendelea kukua hatakuwa mpokeaji anayekaa tu bila kutenda lo lote akiwa
miongoni mwa wenzake. Yampasa kutoa na vile vile kupokea. Matendo yetu mema
huongezeka kwa kuyafanyia mazoezi. Jamii ya Kikristo itatupatia hewa safi ya
kuvuta, na katika kuivuta kwetu hatuna budi kuwa na juhudi. Kazi ya Kikristo
ifanyike, huruma zetu, kuwatia moyo wengine, na mafundisho vitolewe nasi kwa
wale wanaohitaji, kujizuia, upendo, uvumilivu, na ustahimilivu ambavyo
huhitajika, vikitumika katika kazi hii ya Kikristo, vitajenga ndani yetu
wenyewe imani, utii, tumaini, na upendo kwa Mungu wetu.... Ni jambo la maana
ili kuwa na musuli wa kiroho na nguvu kwamba roho iwe na mazoezi. Kazi inapaswa
kufanywa kwa utendaji wa kiroho tukizitumia vizuri nafasi za kufanya mema....
Kadiri mtu anavyozidi kuwa mwaminifu katika kufanya kazi zake za Kikristo,
ndivyo atakavyozidi kuwa mkamilifu....
Udhaifu na kutokuwa na msimamo wo wote
havitatupatia kamwe heshima yo yote katika imani yetu ya Kikristo. Haiwezekani
kuwafikia watu kule waliko na kuwainua juu isipokuwa kama tumaini fulani
limeamshwa ndani yao kwa njia ya uaminifu na utauwa wako. Huwezi kamwe
kuwafikia kwa kushuka chini ya jukwaa hilo la kweli na matengenezo, isipokuwa
kwa kuwaleta wengine juu ya jukwaa hilo ambalo Neno la Mungu limekuandalia
wewe. Iwapo watu wale wanaoipinga imani yetu wanaona kwamba ninyi mnaoikiri
hamna utani, yaani, mko imara, wala hamna tabia mbaya kwa nyakati zote na chini
ya hali zote, na ya kwamba mnakaa ndani ya Kristo, Mzabibu hai, na ya kwamba
ninyi ni wafuasi wa ile kweli na wafanya matengenezo msioyumba, hapo ndipo
mtakapoakisi roho na tabia ile ya Kristo. Katika biashara zenu, katika
ushirikiano wenu na waumini pamoja na wale wasio waumini, katika patakatifu
[kanisani], nyumbani mwenu, na kila mahali, hapo ndipo mtakapoonyesha mvuto wa
upendo wake Mwokozi, ambao utawatawala waumini.
Kipaji, talanta, na fedha sio vya muhimu ili kuweza kuwa na mvuto huo;
lakini jambo la maana ni kwamba wewe ukae ndani yake Kristo, maana kwa njia hiyo
matunda yako yatakuwa ya haki. ----- Letter 1, 1882.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...