UWE NA UWEZO WA KUCHAGUA!
Wala msishirikiane na
matendo yasioyozaa ya giza, bali myakemee. Waefeso 5:11.
Mkristo anapaswa kujitenga mbali na kundi la
wale ambao ni kama mtego kwa roho yake. Unapokutana na wale usioweza kuwainua
katika hali ile ya hewa iliyo safi na takatifu kwa sababu mwelekeo wao wa
kimaadili umepotoka, itakupasa kuwaepuka usishirikiane nao. Watu wa tabaka hiyo
kwa kawaida wana utashi wenye nguvu na tabia inayovutia, na yule adui wa Mungu
anapowashughulikia, wanakuwa mawakala wake wanaofanikiwa sana katika kuziongoza
roho za watu mbali na njia ile ya haki na kwenda katika njia zile za udanganyifu
na za hatari. Hali ya hewa ya kimaadili inayowazunguka watu hao imetiwa waa la
dhambi, nayo inaleta kwa wengine shinikizo la mvuto unaonajisi. ----- YI, Sept.
29, 1892.
Marafiki zako unaoshirikiana nao
hawawezi kutazamiwa kuwa huru mbali na upungufu mwingi katika tabia zao au
dhambi. Lakini katika kuchagua marafiki zako, ungeweka kipimo chako juu sana
kadiri unavyoweza. Namna ya maadili yako yalivyo hupimwa kwa aina ya marafiki
unaowachagua. Epukana na kufanya urafiki wa karibu sana na wale ambao mfano wao
usingechagua kuuiga....
Chagua kuwa marafiki zako wale ambao
wanaiheshimu sana dini na kuyaweka katika matendo yao maongozi yake. Daima weka
mbele yako maisha yale ya baadaye. Marafiki zako wasiondoe mawazo hayo moyoni
mwako. Hakuna kitu kitakachofukuzilia mbali mawazo hayo ya maana kama kuongea
na watu wa ovyo, yaani, wale wasioijali, wala kuipenda dini. Haidhuru wawe
wamefikia kisomo cha juu jinsi gani, kama hawaiheshimu dini, au hawaijali,
basi, hao wasingekuwa marafiki zako wateule. Kadiri tabia zao zinavyovutia kwa
njia zingine, ndivyo kadiri ungeweza kuuogopa mvuto wao kama wenzi wako, kwa
sababu wangekuzungushia mvuto wao usiokuwa wa kidini, wa kikafiri, yaani, usioheshimu
mambo matakatifu, na hata hivyo wanaweza kuuchanganya na mambo yao mengi ya
kuvutia kiasi kwamba itakuwa ni hatari kweli kwa maadili yako. ---- Letter 17,
1878.
Uwe shujaa kama Danieli. Uwe shujaa kusimama peke yako.... Ukimya
unaoletwa na woga mbele ya marafiki zako waovu, wakati wewe unasikiliza hila
zao, hukufanya wewe kuwa mmoja wao.... Uwe na ujasiri kutenda mema. ----- 3BC
1155.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...