"Hakuna ushindi juu ya jambo hili," alisema MICHAEL L. RYAN. "Hakuna washindi wala walioshindwa."
Roho Mtakatifu ameongoza wajumbe wa kikao cha General Conference 2015 kupiga kura ya HAPANA, kuhusu suala la kuwawekea mikono ya wakfu kwa kazi takatifu wanawake.
Rosa T Banks akiwasomea wajumbe wa baraza swali wanalopaswa kulipigia kura muda mchache baadae mara baada ya ombi maalumu kuombea zoezi hilo kutolewa. |
Swali lililopigiwa kura:
Baada ya utafiti wako kwa nja ya maombi katika biblia, maandishi ya Ellen G.White, na taarifa ya tume ya utafiti juu ya kuwekewa mikono ya wakfu kwa kazi takatifu, na;
Baada ya kuzingatia kwako kwa umakini kwamba kipi ni bora kwa ajili ya kanisa na utimilifu wa lengo lake.
Inakubalika kwa kamati ya utendaji ya divisheni kwa namna wanavyoweza kudhani ni sahihi kulingana na maeneo yao, kuwa na vifungu vya kuwekea mikono ya wakfu wanawake kwa kazi takatifu kwenye huduma ya injili? Ndiyo au Hapana
i.e
After your prayerful study on ordination from the bible, the writing of Ellen G. White, and the reports of the study commissions, and;
After your careful consideration of what is best for the church and the fulfillment of its mission,
It is acceptable for division executive commitees as they may deem it appropriate in their territories, to make provision for the ordination of women to the gospel ministry? Yes or No
At the conclusion of the vote the count was as follows:
Hitimisho la kura ziliohesabiwa ilikuwa kama ifuatavyo, waliosema:
At the conclusion of the vote the count was as follows:
- No: 1381
- Yes: 977
- Abstain: 5
- Total: 2363
Hitimisho la kura ziliohesabiwa ilikuwa kama ifuatavyo, waliosema:
- Ndiyo ni 977 sawa na 41% ya waliopiga kura.
- Hapana ni 1381 sawa na 58% ya waliopiga kura.
- Wasiopiga kura ni 5.
- Jumla ya kura zote ni 2363.
MAELEKEZO KABLA YA KUPIGA KURA
Myron akitoa maelekezo yaliyopaswa kuzingatiwa na wajumbe ili kufanikisha zoezi la upigaji kura |
Maelekezo yameendelea kutolewa kama yanavyoonekana katika picha |
ZOEZI LA KUPIGA KURA LIMEANZA
Wajumbe wakiendelea na zoezi la kupiga kura mara baada ya maelekezo kukamilika |
ZOEZI LA KUHESABU KURA LIKIENDELEA
Wajumbe wakidumu kuimba mara baada ya kumaliza kupiga kura huku wakisubiri zoezi la kuhesabu kura likamilike |
Zoezi la kuhesabu kura likiendelea |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...