Alhamisi, 23 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI:- UKUTA WA MOTO DHIDI YA MAJARIBU - Alhamisi, Julai 23, 2015

Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11.
Shetani anatafuta daima kuishawishi mioyo ya wanadamu kwa hila zake.
Yeye ndiye mwanzilishi mwamba; alipewa uwezo huo na Mungu, lakini akauharibu uwezo wake wote mtukufu kwa kuyapinga na kuyafanya mashauri yake yule Aliye juu sana yasiwe na maana yo yote....

Tunaweza tu kushinda kwa kulisadiki kila neno litokalo katika kinywa chake Mungu.
Yatupasa kujua kile kilichoandikwa ili tusishindwe na madanganyo na uchawi wake Shetani....
Iwapo tumenaswa kwa uwezo wake ulio kama uchawi, basi, hebu katika jina lake Yesu na tuukemee uwezo wake, na kujitenga na Shetani pasipo kuchelewa....
Wale wanaomlilia Mungu ili awaokoe kutokana na uchawi wa kutisha ambao Shetani anataka kuwatupia, itawapasa kuyathamini sana Maandiko.
Usalama wetu pekee ni katika kuipokea Biblia nzima, si kwa kuchukua mafungu yale tu yaliyojitenga, bali kwa kuiamini kweli yote.
Miguu yako iko juu ya mchanga unaonyiririka kama wewe unalihafifisha neno moja lililoandikwa.
Biblia ni mawasiliano yatokayo mbinguni, tena ni ujumbe hai kwa ajili ya roho zetu kana kwamba sauti kutoka mbinguni ilikuwa imesikika ikisema nasi.
Kwa kicho gani na heshima na unyenyekevu tungekuja kuyachunguza Maandiko, ili tupate kujifunza mambo yale ya milele....
Hebu kila mmoja na ajifunze Biblia yake, akijua kwamba Neno la Mungu linadumu milele kama kilivyo kiti chake cha enzi ambacho ni cha milele. Kama ukija kujifunza Maandiko kwa unyenyekevu, kwa maombi ya dhati ukitaka uongozi wake, basi, malaika wake Mungu watakufunulia mambo yake yaliyo hai; na kama unazihifadhi kweli hizo, basi, zitakuwa kwako kama ukuta wa moto dhidi ya majaribu, madanganyo, na uchawi wa Shetani....
Neno la Mungu linaweza kuziokoa roho zenu, yaani, kuwafanya mwe na hekima hata kupata wokovu.
Mtunga Zaburi asema hivi, "Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, nisije nikakutenda dhambi."
Basi na tulifiche Neno la Mungu mioyoni mwetu, ili tu"pate kuweza kushindana siku ya uovu, na [tu]kiisha kuyatimiza yote, kusimama."
Waefeso 6:13. ---- ST, Sept. 18, 1893.
.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...