Jumamosi, 11 Julai 2015

"USHINDI WA KURA YA HAPANA DHIDI YA KUWEKEWA MIKONO YA WAKFU WANAWAKE HAIBADILI SERA YA SASA YA KANISA" alisema Rais Ted Wilson

Divisheni ya Amerika ya kaskazini inasema itaendelea kuhamasisha wanawake kutumika katika huduma ya injili.

Rais wa Baraza kuu Ted N.C. Wilson alisema hapo jana kwamba kura iliyopigwa wiki hii kuhusu suala la kuwawekea mikono ya wakfu wanawake ilimaanisha “tumedumisha sera ya sasa.”

Wilson aliwaambia wajumbe katika kikao cha Mkutano Mkuu kura iliyopigwa jumatano ilikuwa kwa ajili ya kuzzuia mgawanyiko wa kanisa katika kufanya maamuzi juu ya kuwawekea mikono wanawake.

Alisema kura hazina uhusiano wowote na wanawake waliokuwa wameteuliwa kama wazee wa kanisa mahalia, tendo lililotokana na sera ya kanisa na kuwepo katika utendaji kwa miongo kadhaa.

Aidha, alisema kura hazikuhusiana na watumishi wateule, ambao wanaweza kuwa wakiume au wakike chini ya sera ya kanisa.

“Hivyo hebu tuwekane sawa kwa kile kilichopigiwa kura siku ya jumatano,” Wilson alisema. “Sasa tunarudi katika uelewa wetu wa awali, na Nina wasisitiza kwa nguvu zote kuhusika na kile kilichopigiwa kura tu. lakini usihusishe katika kura vitu ambavyo havikuwa katika orodha ya kupigiwa kura. Tunahitajika kuwa waungwana, tunahitajika kuwa wawazi na wakweli, na wote tunapaswa kukubali kile kilichopigiwa kura katika kikao cha Mkutano Mkuu.

Wilson aliwaomba viongozi wa divisheni kufafanua maana ya kura iliyopigwa katika maeneo yao.

Muda mfupi mara baada ya Wilison kuongea, Rais wa divisheni ya Amerika ya kaskazini Daniel R. Jackson alitolea ufafanuzi akisema “bila kuzingatia kura za kanisa ulimwenguni.”

Alisema divisheni zilikubali kwamba,"Kura imepiga marufuku divisheni zote 13 za kanisa ulimwenguni au taasisi yoyote ya divisheni hizo katika kufanya maamuzi yao wenyewe juu ya  kuzingatia na utekelezaji wa kuwekewa mikono ya wakfu wanawake katia huduma ya injili.”

Lakini, aliongwza, hoja haikukataza wanawake kutumika kama wachungaji wateule wa; wanawake katika kuhudumu kama wazee wa kanisa mahalia, na mashemasi wa kike.

“Kwa sababu hoja haikukataza hivyo vitu, hivyo basi tunaendelea kuwatia moyo wote ambao wamekuwa wakihudumu katika nafasi hizo kuendelea kutumika,” alisema Jackson.

Aliongeza: “Ni muhimu kuelewa kwamba Divisheni ya Amerika ya kaskazini itaendelea kufuata maelekezo yaliyo katika sera ya utendaji ya General Conference inayoruhusu konference na unioni kuwapatia leseni wanawake kama watumishi wateule katika huduma za kichungaji. Pia tutaendelea kuhimiza kutumia huduma za wanawake kama wazee wa makanisa na mashemasi.”

Wilson siku ya ijumaa pia alisema ameziomba divisheni kuwa waangalifu na makini kuzingatia mambo maalum yanayokuja katika maeneo yao. Hakufafanua zaidi, alisema tu Uongozi wa Baraza kuu unatarajia mambo yataenda vizuri na unategemea kupata msaada kutoka katika divisheni juu ya masuala hayo.

He said division leaders have a spirit of upholding what the General Conference in session votes. Decisions made by the General Conference in session have the highest authority in the church.

Wilson, meanwhile, sought to squash concerns from some church members that a revision to the Church Manual that delegates approved earlier Friday might limit the authority or activities of the General Conference.

“Sababu ya maneno haya ni kuzuia rufaa yoyote kutoka chini kuja juu kupitia utaratibu,” alisema Wilson.

Marekebisho yanazipa divisheni haki ya kuzuia mzozo kutoka ngazi za chini kuja General Conference. Ngazi ambazo rufaa yao inaweza kusikilizwa katika divisheni inahusisha kanisa mahalia, konferensi, na unioni.

Wilson alisema General Conference kwa ujumla inatenda kupitia divisheni na ngazi zake ili kutatua rufaa.

“Hivyo tafadhali usije kudhania vitu ambavyo, kwa maoni yangu, na uelewa wangu, kamwe hayapo huko ,” alisema.
BOFYA HAPA KUPATA TAARIFA KUTOKA KWENYE CHANZO CHA GC

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...