Jumatatu, 13 Julai 2015

KESHA LA ASUBUHI: KIPIMO CHA TABIA - Jumatatu, Julai 13, 2015

Lakini  hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana  na imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. 1 Timotheo 6:9,10.
Shetani  ana nyavu na mitego, kama mitego ile ya mwindaji ndege, yote hiyo imeandaliwa kuzitega roho zetu. Ni kusudi lake lililodhamiriwa kwamba wanadamu wazitumie nguvu zao walizopewa na Mungu kwa makusudi ya kibinafsi kuliko kuzitoa kwa ajili ya kumtukuza Mungu. Mungu angependa wanadamu waingie katika kazi ile itakayowaletea amani na furaha, na itakayowaletea faida ya milele; bali Shetani anatutaka sisi kukusanya juhudi zetu zote na kuzitumia kwa kile kisicho na faida yo yote, yaani, kwa vitu vile vinavyoharibika vikitumiwa. ----- RH, Sept.1, 1910.  Utukufu  wa ulimwengu ule ujao unafunikwa na vitu vile vinavyoharibika vya ulimwengu huu. "Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako." Mathayo 6:21. Mawazo yako, mipango yako, nia yako, vyote vitakuwa na mfumo wa kidunia, na nafsi yako itanajisiwa kwa uchoyo na kujipenda nafsi. "Kwa kuwa itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Marko 8:36. Siku yaja ambayo sanamu za fedha na dhahabu zitatupiliwa mbali kwa fuko na popo, na watu walio matajiri watalia na kupiga yowe kwa sababu ya mashaka yao yatakayowajia.... Iwapo  mawazo yako, mipango yako, makusudi yako, vyote vimeelekezwa katika kujilimbikizia  v itu vya ulimwengu huu, basi, mashaka yako, mafunzo yako, mambo uyapendayo, yatakazwa juu ya ulimwengu huu. Mambo ya mbinguni yanayopendeza sana yatapoteza uzuri wake kwako.... Moyo wako utakuwa pamoja na hazina yako.... Hutakuwa na muda wa kuutenga kando  kwa ajili ya kujifunza Maandiko wala kuwa na maombi ya dhati ili upate kuokoka katika mitego ya Shetani....  Laiti  kama mambo yale ya kuvutia sana ya ulimwengu ule ujao yangethaminiwa! Kwa nini wanadamu hawajihusishi sana na wokovu wa roho zao wakati zilinunuliwa kwa gharama kama hiyo na Mwana wa Mungu? ----- RH, Sept.1, 1910.  Kwa  kudra yake Mungu, baadhi ya watu wanaweza kuchuma mali nyingi kuliko wengine kwa ustadi wao wa kimwili au kwa maarifa yao ya ubunifu. Mungu anawabariki kwa kuwapa mali, busara,  na ustadi ili wapate kupokea mali yake na kuwagawia wengine ambao huenda hawajapata mibaraka hiyo. Kule kuwa na mali kunakuwa ndicho kipimo cha tabia. -----  MS 101, 1906.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...