Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima;
yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
" Yohana 6:35. Ulimwengu unaangamia kwa kuikosa kweli, kweli ile safi, isiyoghoshiwa. Kristo ndiye ile kweli. Maneno yake ndiyo kweli. ----- MS 130, 1897.
Muumini, akiwa katika ushirika wa Roho, anapoishika kweli yenyewe hasa, na kuitumia, anakula mkate [chakula] ule ushukao chini kutoka mbinguni. Anaingia katika maisha yake Kristo, na kuithamini kafara ile kuu iliyotolewa kwa ajili ya wanadamu wenye dhambi.
Maarifa yatokayo kwa Mungu ndiyo ule Mkate [chakula] wa uzima.
Hayo ndiyo majani ya mti ule wa uzima ambayo ni kwa kuwaponya mataifa.
Mkondo ule wa maisha ya kiroho huifurahisha nafsi wakati maneno yake Kristo yanaposadikiwa na kuwekwa katika matendo.
Hivyo ndivyo tunavyofanywa kuwa umoja na Kristo.
Uzoefu wa maisha uliokuwa dhaifu na mnyonge unageuka na kuwa na nguvu.
Ni uzima wa milele kwetu iwapo tunashikamana sana na mwanzo wa ujasiri wetu mpaka mwisho.
Kweli yote haina budi kupokewa kama maisha yake Yesu.
Kweli inatutakasa sisi na uchafu wote, na kuutayarisha moyo kwa ajili ya kuwamo kwake Kristo.
Kristo anaumbika ndani, tumaini la utukufu.
----- MS 103, 1902.
Kweli inapaswa kuliwa kila siku.
Hivyo tunayala maneno yake Kristo, anayoyatangaza kuwa ni roho, tena ni uzima.
Kule kuipokea kweli kutamfanya kila mpokeaji kuwa mtoto wa Mungu, yaani, mrithi wa mbinguni.
Kweli iliyomo moyoni si andiko baridi, yaani, lililokufa....
Kuna furaha kamili ndani ya kweli hiyo.
Kuna utukufu katika maisha ya mjumbe yule wa kibinadamu anayeishi na kufanya kazi chini ya mvuto uhuishao wa ile kweli.
Kweli ni takatifu na tukufu.
Ina nguvu na uwezo kuliko kitu kingine cho chote katika kujenga tabia inayofanana na ile ya Kristo.
Ukihifadhiwa moyoni, upendo wake Kristo ni bora kuliko upendo wa mwanadamu ye yote.
Huo ndio Ukristo hasa. Hivyo kweli hiyo
----- kweli iliyo safi, yaani, isiyoghoshiwa -----
hukaa katika ngome ya mwili wa mwanadamu.
Huo ndio uzima wa Mungu ulio moyoni.
"Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu."
Ezekieli 36:26. ----- MS 130, 1897.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...