Soma Isaya 39:5-7 na Danieli 1:1,2. Je, aya hizi zinahusianaje?
Danieli, ambaye jina lake humaanisha “Mungu ni hakimu wangu” alilazimishwa kutembea toka Yerusalemu, mji uliokuwa umeshindwa, hadi katika mji mkuu wa Babeli. Kitabu cha Danieli hutoa picha kidogo ya maisha yake katika ikulu za Babeli na Uajemi. Baada ya miaka mitatu ya “elimu” huko Babeli, Danieli aliajiriwa kama mtumishi wa serikali na mshauri wa mfalme. Kupitia uweza wa Mungu, alipanda juu kuliko hadhi ya kawaida ya mateka na kuwa mmisionari mstahiki katika yale mataifa makubwa mawili.
Kitabu cha Danieli ni zaidi ya hazina ya uandishi wa kiunabii. Msomaji anakutana na baadhi ya changamoto zilizowakabili Waebrania walioishi katika utamaduni wa kigeni ambao haukuwasaidia kwa utii wao kwa Mungu wa Israeli, na wakati mwingine ukionesha uhasama wa wazi. Pia kitabu hiki hutupatia taswira ya kupendeza ya watu waliojifunza kuishi kwa kiwango cha juu cha ukweli licha ya kutokuwapo hekalu, makuhani, au sadaka za kuteketezwa.
Soma Danieli 1:8-13; 5:12; 6:4; 9:3-19. Je, aya hizi hutuambia nini kuhusu tabia ya Danieli ambayo ilimfanikisha kuwa mmisionari maarufu kama alivyokuwa?
“Kila taasisi yenye jina la Waadventista wa Sabato inapaswa kuwa taa kwa ulimwengu kama Yusufu alivyokuwa Misri, na kama Danieli na wenzake walivyokuwa kule Babeli. Kwa majaaliwa ya Mungu watu hawa walichukuliwa mateka, ili waweze kupeleka maarifa ya Mungu wa kweli kwa mataifa ya kipagani. Walipaswa kuwa wawakilishi wa Mungu katika ulimwengu wetu. Hawakupaswa kufanya mwafaka na mataifa ya waabudu sanamu waliyoishi kati yake, bali walipaswa kusimama thabiti katika imani yao, wakichukulia kuwa ni heshima kubwa kubeba jina la waabudu wa Mungu aliyeumba mbingu na nchi”.-Ellen G.White, Testimonies for the Church, vol. 8, uk. 153.
Fikiria jinsi ambavyo ingalikuwa rahisi kwa Danieli kufanya maridhiano, hasa ukizingatia mazingira aliyokuwamo. Kielelezo chake kinatufundisha nini kuhusu kutofaa mara nyingi kwa visingizio vyetu vya kuhalalisha ufanyaji maridhiano na ulimwengu?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...