SABATO MCHANA |
Sabato Mchana
Somo la Juma Hili: Yona 1-4; 2 Wafalme 14:25; Isaya 56:7; Isaya 44:8; Mathayo 12:40; Ufunuo 14:6-12.
Fungu la Kukariri: “‘Hakika natambua ya kuwa Mungu hana upendeleo; bali katika kila mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yete’” (Matendo 10:34, 35).
Kisa cha Yona ni maelezo kuhusu nabii Mwebrania aliyekuwa akihudumu nje ya eneo alilokuwa analipenda.
Aliishi zama za mfalme Yeroboamu II, mnamo 750 KK (2Wafalme 13: 25), Yona ndiye nabii pekee wa Agano la Kale ambaye tunajua kwamba alitwa moja kwa moja na Mungu kuwa mmishionari katika nchi ya kigeni. Ukweli kuwa Muumbaji wa mataifa yote hakukusudia wokovu ukomee kwa taifa lake teule peke yake, ni jambo lililoelezwa kwa kina katika Agano la kale, hasa katika vitabu vya Isaya na Zaburi, ingawa teolojia ya Waisraeli zama za Yona haikukubali kuwa watu wa Mataifa nao pia wanahusishwa katika mpango wa Mungu wa wokovu. Hata katika zama za Agano Jipya lilikuwa somo gumu kwa Wayahudi kuweza kulipokea.

Katika sura nne za Yona, tunasoma kumbukumbu ya kweli ya uzoefu wa Yona wa kusita kuwa mmisionari wa kwanza katika nchi ya kigeni, yakiwapo mambo ya kutia moyo na pia ya kukatisha tamaa. Hapa tunaona hisia halisi za mtu, itikio la kibinadamu kwa wito wa Mungu, na msisitizo wa hitaji la utume katika nchi za kigeni. Miongozo michache kwa ajili ya utume katika nchi za kigeni na jinsi ya kushuhudia watu wa tamaduni tofauti hujitokeza katika kitabu hiki, ambacho pia hutupatia ufumbuzi kwa baadhi ya masuala na matatizo ambayo yanawakabili wamisionari wa kisa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...