Jumamosi, 4 Julai 2015

KESHA LA ASUBUI: HAKUNA CHA THAMANI MNO USICHOWEZA KUMPA MUNGU, Julai 4, 2025.

Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee. Waebrania 11:17.

Jaribio la Ibrahimu lilikuwa kali mno ambalo lilipata kumjia mwanadamu. Angeshindwa chini ya jaribio hilo, asingeweza kuandikwa kamwe kama babawa wenye imani....

Fundisho hilo lilitolewa lipate kuangaza katika vizazi vyote, ili sisi tupate kujifunza ya kwamba hakuna kitu cho chote cha thamani mno ambacho hatuwezi kumpa Mungu. Ni wakati ule tunapokiangalia kila kipawa kama chake Bwana ili kipate kutumika katika kazi yake,hapo ndipo tunapojipatia ule mbaraka wa mbinguni. Mrudishie Mungu maliyako uliyokabidhiwa, ndipo utakapokabidhiwa mengi zaidi. Tunza mali yako kwa ajili yako mwenyewe, nawe hutaweza kupokea thawabu yo yote katika maisha haya, tena utapoteza thawabu yako katika maisha yale yajayo.... Wako wengi ambao hawajapata kamwe kujisalimisha kabisa kwa Mungu.

 Hawana wazo sahihi juu ya kafara ile isiyokuwa na kifani ambayo ilitolewa na Mungu kuuokoa ulimwengu huu ulioharibika. Endapo Mungu angesema nao kama vile alivyosema na Ibrahimu, wasingeweza kuifahamu sauti yake kiasi cha kutosha kujua kwamba alikuwa anawataka wamtolee sadaka, ili kukipima kina cha upendo wao na unyofu wa imani yao. 

Baa la kujipenda nafsi [uchoyo] huambukiza kama vile ukoma. Wale watakaoingia katika majumba yale ya kifalme ya mbinguni hawana budi kutakaswa kutokana na kila sazo la baa hilo.... Bwana anayo kazi kubwa kwa ajili yetu ili tupate kuifanya, naye anatuita tumtazame Yeye, tumtegemee Yeye, tutembee naye, na kuzungumza naye. Anatualika tuvisalimishe kabisa vyote tulivyo navyo pamoja na sisi wenyewe jinsi tulivyo, ili atakapotutaka sisi kumtolea sadaka, tuwe tayari na tumtii kwa hiari. Tutafurahia utimilifu wa neema yake pale tu tutakapompa vyote Kristo.

 Tutajua tu maana ya furaha ya kweli hapo tutakapoendelea kuuchochea moto unaowaka juu ya madhabahu ya kafara. Mungu atawapa urithi mwingi sana baadaye wale waliofanya mengi sana wakati huu wa sasa.... Kila siku, chini ya mazingira tofauti, anatupima; na katika kilajuhudi ya kweli itokayo moyoni anawachagua watenda kazi wake, si kwa sababu wao ni wakamilifu, bali kwa sababu wako tayari kufanya kazi bila kuwana ubinafsi kwa ajili yake, naye anaona kwamba kwa njia ya kuunganishwa naye wanaweza kupata ukamilifu huo. ----YI, Juni6, 1901

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...