Jumatano, 22 Julai 2015

LESONI JUMATANO, Julai 22, 2015- KIZAZI CHA NINAWI


Somo Yona 3. Ni ujumbe gani muhimu unapatikana hapa katika muktadha wa kushuhudia na uinjilisti?

"Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili,kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa; ukaihubiri habari nitakayokuamuru." (Yona 3:1,2).
Vitenzi viwili ni muhimu hapa. Kwanza, hii ni mara ya pili Mungu kumpatia agizo "Ondoka!" Mungu hakati tamaa. Huwapatia wanadamu wadhaifu fursa ya pili. Hapa tunapata dhana ya utume sawa na ile ya Agano Jipya, yaani, kuwaendea Mataifa, kinyume na mtazamo ule wa kutarajia mataifa ndio waje kwetu.

Kitenzi kingine muhimu ni "tangaza" au "hubiri". Kutangaza neno daima limekuwa ni suala muhimu katika Biblia. Bado ndiyo njia yenye mafanikio katika kueneza ujumbe wa injili. Mungu alimsisitizia Yona kuwa ni lazima uwe ujumbe ninaokupatia. Yaani, ujumbe tunaohubiri lazima uwe ni ule wa Mungu, siyo ujumbe wetu wenyewe, au uliopindishwa, au kubadilishwa, au kupunguzwa ili uendane na utashi wetu.

Ujumbe wa Mungu daima ni tahadhali na ahadi, hukumu na injili. Ujumbe aliokuwa akiutangaza ni: "Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa." (Yona 3:4). Hiyo ilikuwa ni hukumu. Lakini kulikuwa na ahadi ya tumaini, ya ukombozi, ya wokovu (ni lazima kulikuwepo kwani watu walitii ujumbe huo na kuokoka).

Pamoja na "injili ya milele" kuwa ndio kiini chake, Ufunuo 14:6-12 pia hutahadharisha kuhusu hukumu. Injili na hukumu huenda pamoja: injili inatupatia njia ya Mungu ya kuepuka adhabu ambayo hukumu imetamka kuwapatiliza watu wote.

Hakuna mahubiri ya injili yenye kufaa isipokuwa hukumu imefundishwa."Maridhiano," ambayo huongoza katika kulegeza kanuni za msingi na kupunguza umuhimu wa tofauti zilizopo baina ya dini au baina ya mapokeo tofauti ya Kikristo, ni yenye hatari. Japokuwa katika utume tunahitajika kuandaa masomo yetu yafae kwa watu tunaojaribu kuwafikia, kamwe haitupasi kufanya hivyo kwa namna inayohafifisha ujumbe ambao Mungu alitupatia tuutangaze.

Katika Yona 3:5-10, ni nini kilitokea? Watu wa Ninawi waliamini,wakatenda kulingana na kile walichoamini,wakaifanyia mazoezi imani yao, nao wakaokolewa.

Mungu ametupatia ahadi nzuri ajabu, na pia maonyo makali. Je, kisa hiki hutufundisha nini kuhusu masharti ya ahadi na maonyo hayo?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...