Mimi ndimi chakula [mkate] chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele.
Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu....
Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
Yohana 6:51-55.
Maneno haya, "Utupe leo riziki yetu [mkate wetu wa kila siku]," yanamaanisha si chakula tu cha kimwili bali chakula cha kiroho kinachotupatia uzima wa milele kwa yule anayekipokea. Tunaposadiki na kulipokea Neno la Kristo, tunakula mwili wake na kunywa damu yake....
Kama vile kula chakula cha kimwili kunavyoufanya mfumo wa mwili kupata nguvu, hivyo ndivyo kula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu, kunavyoiimarisha tabia ya kiroho.
Neno la Mungu ni roho, tena ni uzima kwa kila mmoja anayelitumia.
Anayekula mwili na kunywa damu yake Kristo anakuwa mshiriki wa tabia yake ya uungu....
Mkondo wenye nguvu, uletao uzima hutiririka kutoka kwa Mwokozi kwenda kwake.
----- MS 48, 1895.
Hakuna ye yote awezaye kula mwili na kunywa damu hiyo kwa niaba ya mtu mwingine.
Kila mmoja sharti aje kwake Kristo akiwa na roho yake yenye njaa, yaani, kila mmoja ni lazima asadiki yeye mwenyewe, ajisikie kuwa anayo haja ya rohoni mwake mwenyewe.
- ---- MS 29, 1896.
Tukijazwa na Mkate huo wa Uzima, hatuwezi kuwa na njaa ya vishawishi vya ulimwengu huu, wala misisimko ya ulimwengu huu, wala utukufu uliomo ulimwenguni humu. Uzoefu wetu wa kidini utakuwa wa aina ile ile kama chakula kile tulacho.
----- MS 50, 1895. Chakula tunachokula katika mlo mmoja hakitutoshelezi [hakikidhi njaa yetu] milele.
Kila siku ni lazima tule chakula hicho.
Kwa hiyo, kila siku yatupasa kula Neno la M ungu ili uzima nafsini mwetu upate kufanywa mpya.
Ndani ya wale wanaokula kila siku Neno hilo, Kristo anaumbika, tumaini la utukufu.
Kupuuzia kusoma na kujifunza Biblia huleta njaa ya kiroho.... Kristo ndiye uzima wetu.
Moyo ule anamokaa utatimiza matakwa ya kanuni zake kwa kumcha yeye kabisa na kujitoa wakf kwa Mungu.
Kristo anapougusa moyo anaujenga, anaupa mahitaji yake yanayorudia tena na tena.
Yeye kwetu anafanywa kuwa hekima na haki na utoshelevu na ukombozi.
Yeye ndiye utoshelevu wetu.... Yeye ndiye uzima unaotiririka kama damu katika moyo wetu.
Iwapo anakaa pamoja nasi, tunaweza kusema, "Lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu."
Wagalatia 2:20. ----- MS 60, 190l.
........................................................
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni
Toa maoni hapa...