Jumamosi, 18 Julai 2015

SABATO YA LEO Julai 18, 2015: "TABIBU WA KWELI WA DHAMBI" hubiri kutoka kwa Mzee Ashery Anthony


WIMBO: Namba  111- TABIBU MKUU

FUNGU KUU:,"Na  kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi , atasamehewa. Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye  haki kwafaa sana akiomba kwa bidii." ( Yakobo 5:15 -16)
Mzee wa Kanisa Ashery Anthony akihubiri katika ibada ya leo

FAFANUZI:

Loleote tunalolifanya basi tulifanye kwa bidii, Ni lazima tufikie katika kuomba kwa bidii ili tuishinde dhambi.

Kumrejeza Yesu katika maisha yetu ni sifa ya kuachana na dhambi, ni lazima sisi wenyewe tujifunze, tuombe kwanza ili wingi wa dhambi uweze kupungua hatimaye kuondoka kabisa. 

Ni lazima pia kufika mahali tuungane katika maombi ya umoja ili kuweza kuponywa dhidi ya dhambi.

Tukifanya kila kitu kwa bidii basi Bwana Yesu Kristo ataturejeza kwake.

WITO

Tujitoe wakifu mbele za Mungu ili kuachana na dhambi, hebu tukubali kujikana nafsi kwa kujitoa kikamilifu mbele za Mungu.
Usiangalie nani anakuangalia bali muangalie Yesu pekee nawe utapata wokovu.

Bwana Yesu Kristo awabariki zaidi na zaidi  Amina!!!




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...