Alhamisi, 23 Julai 2015

LESONI YA ALHAMISI:- KILIO CHA NINAWI - Julai 23, 2015


Yona 4:1-11 huthibitisha kuwa kikwazo kikubwa kwa Mungu kumfanya nabii wake ahusike katika utume kwa ulimwengu hakikuwa umbali, upepo, mabaharia, samaki, au watu wa Ninawi.
Kikwazo kilikuwa ni nabii mwenyewe. Imani ya watu wa Ninawi ilikuwa kinyume na kutoamini kwa Yona na roho yake ya kulipiza kisasi. Katika Maandiko, Yona ndiye mtu pekee aliyemlaumu Mungu kwa kuonesha rehema, huruma, kutokuwa na hasira, wingi wa upendo, na kughairi mabaya. Mtu anaweza kufikiri kuwa watu wengi wangalizitazama sifa hizi za Mungu kwa shukurani.

"Wakati Yona alipogundua kuwa Mungu amekusudia kuuokoa mji, ambao licha ya uovu wake mkuu, waliongozwa kwenye toba ya kweli wakiwa wamevaa magunia na kujipaka majivu, yeye alipaswa kuwa wa kwanza kushangilia kwasababu ya neema ya Mungu ya ajabu; lakini badala yake aliruhusu akili yake kufikiria juu ya uwezekano wa yeye kuchukuliwa kama nabii wa uwongo. Akiwa amejawa wivu kutetea hadhi yake, alipuuza thamani kuu ya roho zilizokuwamo kwenye mji ule uliohukumiwa. Huruma ambazo Mungu alizionesha kwa watu wa Ninawi waliotubu zilimchukiza sana Yona, na alikasirika sana."-Ellen G. White,Prophets and Kings, uk.271.

Soma Yona 4:10,11. Aya hizi hutufundisha nini kuhusu tabia ya Mungu kinyume na asili ya mwanadamu ya dhambi? Kwa nini tushangilie kuwa Mungu wetu, na wala si mwanadamu mwezetu,ndiye hakimu wetu?

Yona alionesha hasira zake mara mbili katika sura ya nne. Alikasirika kwa sababu Mungu alighairi na kuwaokoa watu wa Ninawi wapatao zaidi ya wakazi mia na ishirini elfu. Pia alikasirika kwa vile mtango ulikauka. Kwa ubinafsi wake, nabii huyu alitakiwa kuweka vipaumbele vyake sawasawa.

Mungu alimwagiza Yona kutambua udugu wa wanadamu wote uliojengwa katika ukweli kuwa Mungu ni baba yetu. Nabii alipaswa kutambua kuwa hadhi yake kama binadamu ni sawa na ile ya "watu hawa wa taifa la kigeni," japo walikuwa wakaidi. Je, watu laki moja na ishirini elfu hawakuwa muhimu kuliko mtango?

Soma tena jinsi BWANA alivyomkemea Yona. Ni kwa jinsi gani Bwana anaweza kutukemea kwa jinsi iyo hiyo? Yaani, ni mara ngapi tunajali mambo yetu binafsi, ambayo wakati fulani mengi yanaweza yakawa ni duni mno, kuliko roho zilizopotea ambazo Yesu alimwaga damu yake ili kuwaokoa?

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Toa maoni hapa...